Heshima za mwisho
Maandalizi ya heshima za mwisho kwa wapendwa, ndio huduma za kampuni ya Corona Tanzania Ltd
Asante kwa kutembelea tovuti yetu ya Corona Tanzania Limited.
Kwa muda wa takribani miaka 20 sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya huduma za mazishi ya Corona Tanzania LTD, tumekuwa tukitoa huduma zetu kitaifa (ndani ya nchi) na hata kimataifa (nje ya nchi).
Kampuni yetu imeamua kufungua tovuti hii ya kuuza majeneza, ili kuwarahisishia wanajamii wetu pale wanapopatwa na janga la msiba na kuhitaji jeneza bora na la uhakika.
Kwa kupitia tovuti hii utaweza kuagiza aina ya jeneza unalolihitaji kwa ajili ya mpendwa wako, na jeneza hilo litaweza kukufikia pale ulipo ndani ya aidha siku moja, au, kutegemea na muda huduma inapoagizwa na umbali wa mkoa aliyoko mhusika, baada ya masaa 48.
Kwa wale wakazi wa Dar Es Salaam, tunawakaribisheni ofisini kwetu, maeneno ya Mikocheni, Barabara ya ''Industrial Way Road N0. 80 '' au dukani kwetu, Mtaa wa Kalenga, maeneo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili..
Karibuni!


Tupo kwa ajili yako
Kuwasaidia wateja wetu pale wanapokuwa wanapitia wakati mgumu ndivyo tunavyojitahidi kufanya kwenye kampuni yetu ya huduma za mazishi - Corona Tanzania Ltd -, na ndiyo maana tuna rasilimali nyingi zinazotuwezesha kufanya hivyo.
Wasiliana nasi ili ujifunze kuhusu huduma zetu, na njia zote tofauti ambazo tunaweza kukusaidia wewe na wapendwa wako wakati wa majonzi.
Asante.
Raphael Habiyaremye
Mkurugenzi Mkuu
Corona Tanzania Limited